– Hizi hapa sababu wanazotoa mara nyingi
Unakutana na jamaa katika hafla ya kifahari mjini. Wiki moja baadaye mnapishana katika mkutano wa wanahabari na kubadilishana nambari za simu.
Mawasiliano yanaanza na baada ya muda mfupi, mapenzi yanaanza kuota: sura, maneno matamu na wema wake umekuvutia.
Habari Nyingine: Wakenya wafunzwa mapenzi: wapenzi waeleza kuhusu safari ya mapenzi yao mtandaoni
Kwa sababu hutaki kutumbukia nyongo unafanya uchunguzi na hakika sifa zake ni bomba kazini na mtaani, na isitoshe yeye si mali ya wenyewe.
Deti inayofuata unakubali akupeleke nyumbani kwake, kuzuri ajabu; unatulia tuli na kujipa starehe.
Jamaa anachukua usukani na kukupalilia mahanjamu, huyo anakubeba juu juu hadi chumbani na kuvua kila kitu.
Joto limepanda nyote mnachemka tayari kucheza ngoma wakati ambapo unakumbuka kuwa hamjatembelea VCT kujua hali yake.
Unashika breki na kuitisha kondomu na hapo anakufahamisha kuwa hatumii mpira.
Hizi ndizo baadhi ya sababu anazokupatoa:
Mwili wangu huathiriwa na ulimbo unaotengeneza kondomu (latex)
Ni sababu ya kuzingatiwa lakini kwanini anataka kushiriki ngono na mtu asiyejua hali yake pasipo kondomu?
Mimi ni msafi, sijaathirika
Thibitisho liko wapi? Anajuaje wewe ni msafi?
Kwani huniamini?
Mkumbushe kwamba ndiyo ngoma yenu ya kwanza hivyo suala la kuaminiana halipo.
Haileti raha
Naam, hana shughuli na wewe iwapo hataki kutumiza sharti hilo.
Bakora halitasimama wima nisipotumia mpira
Hilo ni tatizo lake. Kama bakora haliwezi kusimama, wacha ‘litulie’, hata yeye mwishowe atatulia.
Bakora halitoshei kwa mipira
Dah!!! Iwapo halitoshei katika kondomu ambayo ni mpira unaovutika na kupanuka, basi hatatoshei ndani mwako. Ondoka haraka upesi na usiangalie nyuma.
Najua kabisa kujidhibiti sitakutunga mimba
Nani kasema hapa ni mimba tu wazuia? Kuna madhara chungu nzima wajiepushia.
Ndiwe wa kwanza, ukweli/Sijashiriki mapenzi kwa muda
Naam, naam. Je, anajuaje yeye ndiye wako wa kwanza? Isitoshe, utathibitishaje jambo hilo?
Nitawajibika chochote kitakachotokea/mimba
Huyo anakudokezea kwamba anataka kuwa baba, ama atakusaidia kuavya mimba. Muambie kutumia kondomu ni zaidi ya kushika mimba.
Desturi
Hii ndiyo sababu ya kipuuzi kabisa: eti desturi na imani yake haimruhusu kutumia kjondomu. Haraka upesi dada, ondoka.
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI