Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mwimbaji Linah Amnyakuwa Idriss Sultan Kutoka Kwa Wema Sepetu.

post-feature-imageKipindi cha Nyuma Linah sanga aliingia Bifu zito baada ya Kuibiwa Bwana na Wema Sepetu ambapo alilalamika sana kwenye vyombo vya habari hasa Radioni... Hivi karibuni Linah na Mpenzi wa Wema Sepetu Idriss Sultan wanaonekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida kiasa kwamba inasemekati eti ni wapenzi wanapika na kupakuwa kitendo ambacho kinaonyesha ni kama kulipa kisasi kwa Wema....!! Haya Tuache Movie liendeleeee tutawajuza zaidi kinachoendelea.......

BIFU LA ZARI THE BOSS LADY NA HUDDAH MAPYA YAIBUKA,WAKENYA WAJITOSA KUMTETEA HUDDAH,WEMA SEPETU NAYE AJTAJWA



Wakenya wamekuja juu baada ya Dongo la Zari Kumpata Huddah Kuwa ni Nyaku Nyaku, Inasemekana Diamond yupo nchini Kenya ambapo ameenda kupiga Show Mombasa, sasa wadaku wa Kenya wanasema hiyo ndio sababu Zari Huko alipo hapakaliki kwani anahisi Mrembo Huddah atachukua nafasi hiyo Kumnyakuwa Diamond.....
Hivi Ndiyo Wasemevyo Wakenya Wakimtetea Mtu wao Huddah Monroe na kuwaponda Wabongo ambae huwa kazi yao Kuponda tu wakimtaja na Wema Sepetu kuwa Wabongo Wamegive Up Kwake:

JE WAJUA UKIMFANYIA HAYA MPENZI WAKO HATOKUSAHAU KAMWE


post-feature-imageHabari yako ndugu msomaji?  Natumaini u mzima na mwenye afya njema.
 1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.

2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.

3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali

4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.

5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.

6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini

7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.

8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.

9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.

10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia.

MWANAUME ANAYEMKOSESHA USINGIZI SNURA


Staa wa Ngoma ya Chura, Snura Mushi, juzikati alieleza jinsi anavyowewesekea penzi la mwanaume ambaye ni staa mwenzake wa Bongo Fleva lakini hakumtaja. Katika pekuapekua, Wikienda limenyaka jina la staa huyo kutoka kwa mtu wa karibu wa Snura ambaye amedai kuwa ni Raymond au Rayvanny wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

 Sosi huyo ambaye hakutaka kuchorwa gazetini alidai kuwa, Snura amekuwa karibu na Raymond na ukaribu wao ulizidi baada ya kufanya video ya msanii huyo ya Natafuta Kiki ambapo ndani yake walionesha mambo yao ya chumbani kama mapichapicha yanavyoonesha mitandaoni. “Kama mnakumbuka Snura alitangaza kuwa kati ya majina matano ya wanaume maarufu wa muziki Bongo, yupo mmoja anayemuwewesekea, jina la Raymond lilikiwemo.
“Baada ya video ya Natafuta Kiki, mapichapicha yalianza kumwagwa lakini unaambiwa kuna picha nyingine ambazo haziwezi kuwekwa gazitini kwani ni balaa na kwenye video picha hizo hakuna,” alitonya mnyetishaji huyo.

WEMA SEPETU AJITOSA RASMI BIFU LA MAN FONGO NA MAMA YAKE,AFUNGUKA MAZITO


Leo ni siku ya 3 ya muendelezo wa sakata zito ambalo lime make headlines kinoma katika mitandao ya kijamii.
Ni sakata linalo muhusisha mama mzazi wa mwanadada Wema Sepetu na msanii mchanga ambaye amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa kufanya muziki wa kisingeli (Man Fongo).Jana tuliweza kuyasikia mapovu ya Mama Wema na mgomvi mwenzie Man Fongo ila leo Gossip MasterSoudy Brown ameamua kumvutia waya ambaye anaseekana ndio chanzo cha sakata hilo Sholo Mwambana amefunguka ya kwake.Lakini hapo jana mwanadada Wema alipoona kama mama yake anakuwa ni gumzo sana katika mitandao ya kijamii akaona isiwe kesi ngoja amvutie waya Soudy Brown na kumwambia kuwa aachane na hizo mambo za kumchoresha mama yake.Ni mapovu sio ya kitoto yamemtoka Bi Dada Wema Sepetu na amekana kabisa yeye kumjua Man Fongowakati siku chache zilizopita alipost katika account yake ya Snapchat akiwa anaserebuka na ngoma ya “Hainaga Ushemeji”.
Isiwe kesi ngoja nikupe nafasi ya kuitazama na kusikiliza hii video yenye ubuyu wote unaokiki town kwa sasa.

MWANAFUNZI WA MIAKA 13 AJIFUNGULIA DARASANI, SOMA HAPA


Mwanafunzi alizaa ghafla akiwa shuleni Naivasha.

Msichana wa shule ya msingi aliwashtua waalimu na wanafunzi wengine baada ya kujifungua akiwa shuleni

– Mwanafunzi huyo wa miaka 13 hakuwa na dalili za ujauzito. Alijifungua katika makao ya shule bila usaidizi na kusemekana kupata majeraha.Msichana wa shule ya msingi aliwashtua waalimu na wanafunzi wengine baada ya kujifungua akiwa shuleni

Wanafunzi na walimu walishangaa hasa kutokana na kuwa mwanafunzi huyo hakuonekana kuwa mjamzito.

Mwanafunzi huyo wa umri mdogo aliumia baada ya kujifungua peke yake. Alipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Naivasha punde baada ya walimu kugundua kilichokuwa kimeendelea.

Mwanawe alifariki baada ya masaa kumi na mawili.

“Kulikuwa na hatari kubwa ambapo alijeruhiwa wakati wa kujifungua, alipata matatizo mengine pia alipokuwa akijifungua,” alisema daktari.

Madaktari walisema mtoto alifariki kutokana na matatizo ya kupumua

TAARIFA KUHUSU MAJERUHI 50 WA BODABODA.. SOMA HAPA

 
WASTANI wa Sh milioni mbili zinatumika kumtibu majeruhi mmoja wa pikipiki, jambo ambalo limezifanya hospitali zinazowapokea majeruhi hao, kuzidiwa na gharama hizo za matibabu.


Madaktari kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wamesema kwamba kwa sasa kila siku, wanapokea wastani wa majeruhi kati ya 50 na 60, jambo ambalo linaiwia vigumu taasisi hiyo kutoa huduma za uhakika kwa majeruhi hao.

Gharama hizo zinatokana na vyuma vinavyotumika kuwatibu majeruhi wa mifupa mirefu kuagizwa nje ya nchi, jambo ambalo linaelezwa na madaktari kwamba kutokana na idadi ya majeruhi kuongezeka kila siku, inailazimu MOI kukabiliwa na upungufu wa vifaa hivyo.

Kutokana na kuongezeka kwa majeruhi hao wa bodaboda, Jumuiya ya Madaktari Wakristo (TCMA) wametumia mkutano wao wa mwaka uliomalizika juzi, kujadili jambo hilo na kueleza kuwa ajali zinazotokana na bodaboda ni janga la taifa kutokana na kuziongezea gharama za upasuaji hospitali.

Kwa hali hiyo, wameziomba mamlaka za masuala ya usalama barabarani, kuhakikisha zinatunga sheria kali zitakazowabana wapanda na waendesha bodaboda ili kuepusha taifa kuwa na walemavu wengi wa ajali za vyombo hivyo vya usafiri.

Madaktari kutoka MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, walisema taasisi hiyo kwa sasa imelemewa na majeruhi wa bodaboda, jambo ambalo linafanya vifaa na miundombinu ya taasisi hiyo, kutotosheleza mahitaji na hivyo kufanya gharama zinazotolewa kwa majeruhi hao kuwa hafifu.

Madaktari hao katika mkutano wao wa mwaka wa 79 ambao ulimalizika juzi kwenye ukumbi wa AMECEA, Dar es Salaam, waliwaita wadau mbalimbali wakiwemo madereva wa bodaboda, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), polisi wa Usalama Barabarani, madaktari, maofisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na waandishi wa habari, kujadili namna gani taifa linaweza kupunguza ajali za bodaboda.

Rais wa TCMA, Dk Isaya Tosiri alisema wamelazimika kutumia mkutano huo kujadili ajali zinazotokana na bodaboda kwa sababu hospitali ambako wanafanya kazi madaktari hao Wakristo zimelemewa kutokana na kupokea majeruhi wengi wa pikipiki.

"Kwa kweli hospitali zetu za makanisa zinapokea sana majeruhi wengi wa bodaboda, kila daktari aliyeko hapa analalamika kuongezeka kwa majeruhi huku hospitali zetu hazina uwezo wa kuhimili ongezeko hili, ndio maana tunasema ni janga la taifa ni lazima wadau watafute suluhisho," alisema Dk Tosiri.

Daktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, Yohana Masota iliyoko mkoani Tabora alisema katika hospitali yake wanapokea wastani wa majeruhi 10 kila siku ambao wanatokana na ajali za pikipiki jambo ambalo linafanya hospitali hiyo kuwa na mzigo wa kutibu majeruhi.

"Naamini kwamba ajali nyingi zinatokana na madereva hawa kutokuwa na uelewa wa sheria za barabarani ndio maana wanapata ajali mara kwa mara, ni lazima hatua zichukuliwe maana hospitali zetu zinalemewa," alisema Dk Masota.

Daktari Bingwa wa MOI, Victoria Munthali amesema zamani kabla ya kuruhusiwa kwa bodaboda kubeba abiria wa biashara, taasisi yake ilikuwa inapokea majeruhi wasiozidi watano kwa siku na siku ambako kuna ajali ya basi waliweza kupokea wastani wa majeruhi 10 kwa siku.

"Lakini siku hizi tunapokea wastani wa majeruhi kati ya 50 na 60 kwa siku, miundombinu ni ile ile hivyo uwezo wetu wa kuwahudumia unakuwa mdogo," amesema Dk Munthali.

Ameongeza kuwa hata vifaa kama vyuma, ambavyo ndivyo vinavyotumika kuwatibu majeruhi wa mifupa mirefu, kifaa cha gharama za chini kinauzwa dola za Marekani 70 (takribani Sh 147,000)

"Kwa wale ambao wanavunjika mgongo 'screw' zinazotumika kuwatibu ya gharama za chini ni dola za Marekani 200 (sawa na Sh 420,000).

Dk Boniface Respicious ambaye ni daktari bingwa wa mifupa wa MOI, alisema gharama za kumtibu majeruhi mmoja wa ajali ya bodaboda ni Sh milioni 2 jambo ambalo limefanya hospitali nyingi kulemewa na mzigo wa majeruhi.

Amependekeza kuanzishwe mfuko maalumu wa majeruhi kama ilivyo kwa mifuko mingine ya umeme vijijini (Rea) ambao utasaidia kutibiwa kwa majeruhi wa ajali za bodaboda na magari.

Alisema fedha za mfuko huo zikatwe wakati mmiliki wa gari au bodaboda anapoenda kukata leseni ya matumizi ya barabarani kama inavyofanyika sasa kwa Zimamoto.

"Hizi kampuni za bima hazisaidii lolote kwenye matibabu wakati wanachukua fedha nyingi, nadhani ukianzishwa mfuko wa majeruhi utaisaidia serikali kuwa na fedha za kutosha za kutibu majeruhi na itasaidia kupunguza mzigo ulioko kwenye hospitali zetu," alisema Dk Respicious.

Alisema kwa sasa huduma za kuwatibu majeruhi zimedorora katika hospitali nyingi kutokana na kukosa fedha za kununulia vifaa pamoja na dawa kutokana na ongezeko la majeruhi wa bodaboda.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii, Dk Josphine Ballati alisema vifo vinavyotokana na ajali za bodaboda ni nyingi kuzidi vifo vinavyosababishwa na baadhi ya magonjwa.

"Huu ni ugonjwa mwingine ambao taifa letu limepata, lazima tutafute suluhisho."

Alionya kuwa kama taifa halitachukua hatua, miaka 20 ijayo nguvu kazi nyingi za taifa watakuwa ni walemavu kutokana na usafiri wa bodaboda kutumiwa na watu wengi. Alisema pia hatua zichukuliwe, kuhakikisha zinalipunguzia gharama taifa kuwatibu majeruhi hao.

Mkurugenzi wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano alisema imekuwa ngumu kuwadhibiti madereva wa bodaboda kwa sababu vijana wengi wanaofanya biashara hiyo ni wale ambao walikuwa na tabia za ajabu huko nyuma.

"Hawa ni vigumu kujifunza na kama wakijifunza ni ngumu kuelewa," alisema Kahatano na kusisitiza kuwa serikali inafanya jitihada kufanya usafiri huo baadaye uwe na heshima na kupunguza matatizo ya sasa
Powered by Blogger.
© Copyright Mtanzania forum
Back To Top